99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Maelfu ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha California wagoma wakidai mishahara ya juu, mazingira bora ya kazi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2022
Maelfu ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha California wagoma wakidai mishahara ya juu, mazingira bora ya kazi
Watu wakishiriki katika maandamano kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) huko Los Angeles, California, Marekani, Novemba 14. 2022. (Xinhua)

LOS ANGELES - Makumi ya maelfu ya wafanyakazi wa taaluma katika Chuo Kikuu cha California (UC) huko Marekani wamegoma Jumatatu wakidai mishahara ya juu na mazingira bora ya kazi.

Takriban wafanyakazi 48,000 wa taaluma katika kampasi 10 za Chuo Kikuu cha California wamegoma kufanya kazi Jumatatu asubuhi, limeripoti gazeti la Los Angeles Times, huku likieleza kuwa wafanyakazi hao wa taaluma hufanya kazi nyingi za kufundisha na utafiti katika mfumo mkuu wa elimu ya juu huko California.

Mgomo huo wa kimfumo unajumuisha wasaidizi wa kufundisha, wasomi wa baada ya masomo ya uzamivu, wanafunzi watafiti, wakufunzi na walimu, pamoja na wafanyakazi katika Maabara ya Taifa ya Lawrence Berkeley, na unatarajiwa kusababisha usumbufu mkubwa katika masomo na maisha ya kila siku ya chuo, inasema habari hiyo.

Chuo Kikuu cha California, chuo kikuu cha umma kinachoongoza kwa utafiti wa umma nchini humo, kina zaidi ya wanafunzi 280,000 na kitivo na wafanyakazi 227,000 siku hizi.

Chuo hicho kimesema kwenye wavuti yake rasmi kwamba kwa sasa kiko katika mazungumzo ya mkataba na United Auto Workers (UAW), taasisi inayowakilisha vikundi vya wafanyakazi wa kitaaluma wa chuo hicho katika vitengo vinne tofauti vya mazungumzo: wasomi wa baada ya masomo ya uzamivu, watafiti wa taaluma, wanafunzi wa taaluma waajiriwa (wasaidizi wa kufundisha / wasomaji / wakufunzi), na watafiti wanafunzi.

UAW inakitaka Chuo Kikuu cha California kuongeza mishahara ili wafanyakazi wasilazimike tena kuishi kwa kile walichoelezea kuwa ni kama "mishahara ya umaskini," imeripoti KTLA, kituo kikuu cha televisheni cha Los Angeles.

"Mfumuko wa bei umeathiri katika mapato yetu kwa kiasi kikubwa," Mwakilishi wa Walimu/Umoja wa Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) Michael Dean amenukuliwa akisema kwenye kituo hicho cha televisheni, na kuongeza kuwa mapendekezo yaliyotolewa na chuo kikuu hicho hadi sasa hata hayalingani na kiwango cha mfumuko wa bei na ni "sawa na kiasi cha kupunguzwa kwa mshahara halisi."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha