

Lugha Nyingine
Uturuki yakamata watuhumiwa wa shambulizi la mabomu mjini Istanbul (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2022
![]() |
Tarehe 14, Novemba, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Soylu akiweka maua ili kutoa rambirambi zake kwenye eneo la mlipuko wa mabomu kwenye Mtaa wa Istiklal karibu na Uwanja wa Taksim, katikati mwa Istanbul. (Mpiga picha: Shadati/Xinhua) |
Shirika la Habari la Anadolu la Uturuki lilitoa habari ikisema kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Soylu aliviambia vyombo vya habari tarehe 14 kwamba watuhumiwa waliofanya shambulizi la mlipuko wa bomu katikati mwa Istanbul siku iliyopita walikamatwa na polisi.
Soylu alisema amri ya kufanya shambulizi hilo inawezekana kutolewa na Chama cha Wafanyakazi cha Kurdistan na "Kikosi cha Ulinzi wa Umma " cha jeshi la wakurdi la Syria, ambavyo vimeorodheshwa kuwa kundi la kigaidi na serikali ya Uturuki. Uturuki itachukua hatua kwa shambulio hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma