

Lugha Nyingine
Ndoto ya mchezo wa soka ya Watoto vijijini huko Liujiang, China (2)
Usiku wa tarehe 12, Novemba, 2022, kwenye kijiji cha Taixiaoping cha mji wa Liuzhou, Mkoa wa Guangxi wa China, kwa mara ya kwanza uwanja wa soka unaowasha taa ulitumika na watoto zaidi ya 30 vijijini walifanya mazoezi kucheza mpira wa miguu kwenye uwanja wa soka wenye nyasi.
Mwanzoni mwa mwaka huu, kochi wa soka wa Liuzhou walijitolea kwenda Kijiji cha Taixiaoping, na kuwafundisha bure watoto wa Kijiji hicho kucheza mpira wa miguu wakati wa wikendi. Kwa sababu ya kukosa uwanja unaofaa, watoto waliweza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mpira wa kikapu tu, na wengine wao huanguka na kujeruhiwa. Kuanzia mwezi Julai mwaka huu, kutokana na mashauri ya kamati ya kustawisha kijiji ya Taixiaoping, vijiji wamekusanya zaidi ya Yuan 80,000 kwa ajili ya kujenga uwanja wa soka kijijini. Baada ya uwanja huo kukamilika, wafadhili wengine walitoa nyasi za uwanja wa soka, taa na vifaa vingine kwao, ili watoto vijijini wawe na uwanja wa soka wenye taa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma