

Lugha Nyingine
Mikutano ya ASEAN yahitimishwa, na kupata matokeo yenye matunda kwa ushirikiano wa kiuchumi (2)
![]() |
Waziri Mkuu wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen akizungumza kwenye hafla ya kufunga Mikutano ya kilele ya 40 na 41 ya ASEAN na Mikutano Husika ya ASEAN huko Phnom Penh, Cambodia, Novemba 13, 2022. (Xinhua/Zhu Wei) |
PHNOM PENH - Mikutano ya kilele ya 40 na 41 ya Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na Mikutano Husika ya ASEAN ilihitimishwa nchini Cambodia siku ya Jumapili, na kupata matokeo yenye manufaa kwa ushirikiano mkubwa wa kikanda kuelekea ufufukaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii baada ya janga la UVIKO-19.
"Ndani ya siku hizi nne, tumekuwa na majadiliano ya kina na yenye tija juu ya njia ya kusonga mbele ili kuimarisha msingi mkuu wa ASEAN na thamani yetu katika uhusiano na washirika wetu wa nje, haswa wakati Dunia inakabiliwa na masuala ya changamato yanayobadilika kwa kasi ya kikanda na kimataifa." Waziri Mkuu wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen amesema katika hafla ya kufunga mikutano hiyo.
Jumla ya nyaraka 70 za matokeo na matamko yanayohusu nguzo tatu za jumuiya za ASEAN yalipitishwa na kubainishwa katika mikutano hiyo, na mifumo mbalimbali ya ushirikiano na washirika wa mazungumzo kuidhinishwa, amesema waziri mkuu huyo.
“Tumetoa Taarifa ya Pamoja ya kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la Mwenendo wa Wadau katika Bahari ya China Kusini (DOC) kuadhimisha miaka 20 tangu kusainiwa kwa DOC Mwaka 2002,” amesema.
Ameongeza kuwa, kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya ASEAN, mikutano hiyo imepitisha Taarifa ya Viongozi wa ASEAN kuhusu Maadhimisho ya Miaka 55 ya ASEAN, Tamko la Maono ya Viongozi wa ASEAN kuhusu ASEAN Kushughulikia Changamoto Pamoja (A.C.T), na Taarifa ya Viongozi wa ASEAN kuhusu Ajenda ya muunganisho wa ASEAN baada ya Mwaka 2025.
Siku ya Ijumaa, viongozi wa ASEAN walikubaliana kimsingi kukubali Timor-Leste kuwa mwanachama wa 11 wa ASEAN, kwa mujibu wa taarifa ya viongozi wa ASEAN.
"Ningependa kusisitiza kwamba msingi mkuu wa ASEAN ndiyo nguvu kuu ya mazungumzo na ushirikiano na washirika wetu wa nje kupitia mifumo mbalimbali inayoongozwa na ASEAN," Hun Sen amesema. "Tunadumisha umoja wa ASEAN bila kujali hali kwa manufaa ya eneo zima."
Amesema kustawisha mshikamano na umoja kutaendelea kuwa kipaumbele kikuu cha ASEAN katika miaka ijayo.
Katika hafla hiyo ya kufunga, Hun Sen alimkabidhi ishara ya Uenyekiti wa ASEAN Rais wa Indonesia Joko Widodo ambaye atakuwa ni mwenyekiti anayefuata wa ASEAN.
Widodo amesema akiwa kama mwenyekiti wa ASEAN Mwaka 2023, Indonesia itafanya "Masuala ya ASEAN: Kitovu cha Kukua kwa Uchumi" na kwamba umoja huo lazima uwe eneo la amani na mhimili wa utulivu wa kimataifa, "usiwe wakala wa mamlaka yoyote."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma