

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China atembelea maonyesho ya mabadilishano ya urithi wa kitamaduni kati ya China na Cambodia, ashiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi wa kitamaduni
SIEM REAP, Cambodia - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang Alhamisi asubuhi ametembelea maonyesho yanayoadhimisha miaka 30 ya mabadilishano ya urithi wa kitamaduni na ushirikiano kati ya China na Cambodia huko Siem Reap.
Pia alitembelea maonyesho yanayoadhimisha miaka 30 ya mabadilishano ya urithi wa kitamaduni na ushirikiano kati ya China na Cambodia huko Siem Reap. Katika zaiara hiyo, Li aliandamana na Mwakilishi Mkuu wa Waziri Mkuu wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen na Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia Chea Sophara.
Wziri mkuu Li alipata fursa ya kusikiliza mada kuhusu ushirikiano unaoendelea kati ya China na Cambodia katika uwanja wa urithi wa kitamaduni, na kutazama kwa shauku kubwa maonyesho hayo ya kitamaduni. Aliuliza kuhusu mbinu na vifaa vya ujenzi vilivyotumika katika kukarabati mabaki ya kitamaduni na hatua zilizopitishwa kwa ajili ya kuhifadhi urithi wa kitamaduni, pamoja na mabadilishano na ushirikiano wa kimataifa juu ya urithi wa kitamaduni.
Katika hotuba yake kwenye hafla ya makabidhiano hayo, waziri mkuu Li amesema kuwa imepita miaka 30 tangu China na Cambodia zianze ushirikiano wa urithi wa kitamaduni.
Akiweka bayana kuwa kufundishana na kufanuya ushirikiano jumuishi kati ya ustaarabu vimepiga hatua kubwa katika maendeleo ya binadamu, Waziri Mkuu Li amesema China na Cambodia zote zina historia iliyotukuka na utamaduni wa ajabu, kufundishana kwa pande zote kumechangia ukuaji mzuri wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili na uelewa na maarifa ya watu wa pande hizo mbili na maarifa ya watu kuhusu nchi na utamaduni wa kila mmoja wao vimeweka msingi thabiti wa urafiki baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu Li amesema, mwingiliano kati ya watu wa pande hizo mbili siyo tu kwamba unaleta pamoja tamaduni mbalimbali, lakini pia mioyo ya watu, huku akiongeza kuwa yote haya yana jukumu muhimu kwenye hali ya sasa katika kuweka minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi kuwa thabiti na isiyozuiliwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma