99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mradi wa uwanja wa ndege unaojengwa na China nchini Cambodia wasaidia kuimarisha ujuzi kwa vipaji vya wenyeji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2022
Mradi wa uwanja wa ndege unaojengwa na China nchini Cambodia wasaidia kuimarisha ujuzi kwa vipaji vya wenyeji
Picha hii iliyopigwa Tarehe 8 Novemba 2022 kutoka angani ikionyesha eneo la ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Phnom Penh katika Jimbo la Kandal, Cambodia. (Xinhua/Zhu Wei)

KANDAL, Cambodia - Hang Amatak, mhandisi wa Cambodia mwenye umri wa miaka 30, anajivunia kufanya kazi na kampuni ya China kujenga uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Phnom Penh, akisema kuwa kazi hiyo ni muhimu katika kusaidia kunoa ujuzi na utaalamu wake.

Alipohitimu Shahada ya Uzamili ya uhandisi wa ujenzi kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China Mwaka 2018, Amatak alijiunga na kampuni ya China Construction Third Engineering Bureau ili kujenga uwanja wa ndege wa kiwango cha 4F, daraja la juu zaidi duniani katika Jimbo la Kandal, umbali wa karibu kilomita 20 Kusini mwa mji mkuu Phnom Penh mapema Mwaka 2020.

Akiwa alianza kazi yake kwa cheo cha mhandisi muunganishaji, Amatak amepandishwa cheo hadi cheo cha msaidizi wa kiongozi wa mradi baada ya kufanya vyema kazi alizokabidhiwa.

"Katika usimamizi wa mradi huo mkubwa, ninahisi kwamba nitaweza kusaidia Cambodia katika siku zijazo kwa uzoefu niliojifunza kutoka kwa mradi huu," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua. "Mradi huu wa uwanja wa ndege wa kimataifa umetoa manufaa makubwa kwa wahandisi wetu wa Cambodia, kutupa ajira na uzoefu muhimu."

Mradi huo mkubwa ni matunda ya ushirikiano wa karibu kati ya Cambodia na China chini ya mfumo wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

"Ninajivunia sana kufanya kazi kwenye mradi mkubwa kama huu nchini Cambodia na kuwa sehemu muhimu ya mradi huu," amesema. "Katika siku zijazo, nitakapopata watoto, watajivunia kuwa nimesaidia kuendeleza mradi huu."

Amatak pia amewasifu wahandisi wa China na wafanyakazi wenye ujuzi kwa bidii yao na kujitolea kwao kwa ufanisi katika mradi huo, akisema kuwa amejifunza mengi kutoka kwao.

Ukiwa na ukubwa wa eneo la hekta 2,600 katika majimbo ya Kandal na Takeo, uwanja huo mpya wa ndege unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi Kusini Mashariki mwa Asia.

Sin Chansereyvutha, Msaidizi wa Mkuu wa Sekretarieti ya Idara ya Usafiri wa Anga ya Cambodia, amesema uwanja huo mpya wa ndege wa kimataifa wa Phnom Penh utachukua jukumu muhimu katika kukuza ukuaji wa uchumi na utalii wa Cambodia utakapoanza kutumika.

“Kiwanja hiki kipya kitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 13 kwa mwaka katika kipindi cha muda mfupi na wa kati hadi Mwaka 2030, na hadi kufikia abiria milioni 30 kwa muda mrefu kuanzia Mwaka 2030 hadi 2050,” amesema.

Ujenzi wa muundo mkuu wa eneo la abiria la uwanja huo wa ndege sasa umekamilika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha