

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Cambodia kuhusu kuimarisha ushirikiano wa pande mbili
PHNOM PENH - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amefanya mkutano na Waziri Mkuu wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen Jumatano kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana.
Waziri mkuu Li amebainisha kuwa China na Cambodia zinafurahia urafiki wa jadi wa kina, kiwango cha juu cha kuaminiana kisiasa, na ushirikiano wenye manufaa wa vitendo katika sekta mbalimbali.
“Mwaka 2016, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara yenye mafanikio nchini Cambodia. Mnamo mwaka wa 2020, Xi alimtunukia Malkia wa Cambodia Mama Norodom Monineath Sihanouk tuzo ya nishani ya Urafiki wa Jamhuri ya Watu wa China,” Waziri mkuu Li amesema, na kueleza kuwa matukio yote mawili yaliashiria ukurasa mpya wa urafiki kati ya China na Cambodia.
Waziri mkuu Li amesema China inaipongeza Cambodia kwa maendeleo yake mapya ya kiuchumi na kijamii na kuongeza kuwa China inaziona nchi zote, bila kujali ukubwa wao, kuwa ni sawa na kusisitiza kuwa nchi zote zinapaswa kuzingatia madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
“China inaunga mkono Cambodia katika kuchukua njia ya maendeleo inayokidhi mazingira yake ya kitaifa na kuchukua jukumu muhimu zaidi kwenye majukwaa ya kimataifa na kikanda,” Li amesema.
Waziri Mkuu Li ameeleza kuwa mwaka ujao utashuhudia kutimia kwa miaka 65 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa itakuwa fursa nzuri kwa nchi hizo mbili kufanya shughuli mbalimbali chini ya Mwaka wa Urafiki wa China na Cambodia kuwa wa mafanikio.
Amesema, China iko tayari kuunga mkono Cambodia katika kilimo kinachoendeshwa kwa teknolojia na viwanda, na itaongeza uagizaji wa bidhaa bora za kilimo za Cambodia, kusukuma mbele miradi mikubwa, na kuunga mkono Cambodia katika kuharakisha ukuaji wa viwanda.
“Nchi hizi mbili zitaimarisha ushirikiano katika sayansi na teknolojia, elimu na utamaduni, na kuongeza usafiri wa ndege wa moja kwa moja,” Li amesema, huku akiongeza kuwa China inakaribisha wanafunzi wa Cambodia kusoma nchini China.
Huku akisisitiza kwamba Cambodia yenye utulivu na ustawi ina umuhimu mkubwa kwa utulivu wa kikanda, maendeleo na ukuaji wa uhusiano kati ya China na Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), Li amesema kuwa China inaunga mkono kikamilifu ASEAN na jukumu lake katika kuhimiza amani na maendeleo ya kimataifa na kikanda.
Kwa upande wake, Hun Sen amesema kuwa Cambodia na China ni marafiki wa nguo za chuma na urafiki wa pande mbili unaidhinishwa na kuungwa mkono na watu wa Cambodia, akiongeza kuwa kuna mengi zaidi ya kufanya katika kuendeleza ushirikiano wa Cambodia na China.
Kabla ya mkutano huo, Hun Sen alifanya hafla kubwa ya kumkaribisha waziri kuu Li Keqiang katika Ikulu ya Amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma