99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wamarekani wapiga kura kuchagua wawakilishi kwenye mabunge katika uchaguzi wa katikati ya muhula wenye mvutano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2022
Wamarekani wapiga kura kuchagua wawakilishi kwenye mabunge katika uchaguzi wa katikati ya muhula wenye mvutano
Mpiga kura akijaza karatasi yake ya kupiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko New York, Marekani, Novemba 8, 2022. (Xinhua/Liu Yanan)

WASHINGTON, - Wapiga kura wanaohusika kote nchini Marekani Jumanne wamepiga kura zao katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Mwaka 2022 huku kukiwa na ushabiki na migawanyiko.

Viti vyote 435 vya Bunge la Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) vinawaniwa, kama ilivyo kwa viti 35 kati ya 100 vya Bunge la Seneti. Zaidi ya hayo, majimbo 36 kati ya 50 na maeneo matatu ya Marekani yanachagua magavana. Chaguzi nyingine nyingi za majimbo na za mitaa pia zinafanyika.

Uchaguzi huo unakuja huku Marekani ikikabiliana na mfumuko wa bei na bei ya juu ya gesi, pamoja na wasiwasi kuhusu mdororo wa kiuchumi. Matatizo mengine makubwa kwa wapiga kura ni pamoja na utoaji mimba, uhalifu, sera ya bunduki, na uhamiaji, miongoni mwa mambo mengine.

Mpiga kura wa chama cha Republican anayeishi Virginia ambaye amejitambulisha kwa jina moja tu la George ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba ana wasiwasi kuhusu uchumi wa Marekani na kukikosoa Chama cha Democrats, akisema kuwa ajenda yake imeathiri vibaya nchi.

Kwa Leinaala Zettlemoyer, mfuasi wa Chama cha Democrats kutoka Pennsylvania, haki za wanawake ni suala muhimu zaidi kwake kwenye uchaguzi huu wa katikati ya muhula. Pia ameonyesha wasiwasi wake kuhusu mgawanyiko katika siasa za Marekani na jamii.

 

Zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura wa Marekani wanafikiri kwamba Marekani inaelekea kwenye njia mbaya, kwa mujibu wa matokea ya kura ya maoni ya kitaifa ya NBC News ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Mwaka 2022 yaliyotolewa Jumapili.

Kura hiyo ya maoni imeonesha kuwa asilimia 81 kwa pamoja wanasema "hawaridhiki" sana au "kwa kiasi fulani" na uchumi wa nchi.

Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye hagombei katika uchaguzi huu wa katikati ya muhula, siku ya Jumanne, aliandika jumbe mfululizo kwenye mtandao wa Twitter akielezea kile anachokizingatia mafanikio ya serikali yake huku akionya kuhusu juhudi zinazowezekana za Republican kurudisha nyuma mafanikio hayo.

Rais wa zamani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari nje ya eneo la kupigia kura huko Palm Beach, Florida, kwamba amempigia kura Gavana Ron DeSantis, ambaye anawania muhula wa pili.

Trump, ambaye mara kwa mara amedokeza nia ya kugombea tena Ikulu ya Marekani, White House Mwaka 2024, alisema Jumatatu kwamba atakuwa na "tangazo kubwa sana" linalokuja Novemba 15 katika eneo lake la Mar-a-Lago huko Florida.

"Kwa ujumla, Marekani na wapiga kura wake wako katika hali mbaya sana," mtafiti mashuhuri wa Marekani John Zogby aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika mtandaoni mwezi uliopita. "Kutakuwa na watu tofauti wanaolaumu watu tofauti."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha