99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mjumbe wa China azitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi za ufadhili wa tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2022
Mjumbe wa China azitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi za ufadhili wa tabianchi
Mjumbe Maalum wa China wa Mabadiliko ya Tabianchi Xie Zhenhua akihutubia katika Mkutano wa kilele wa Utekelezaji wa Hatua za Tabianchi kwenye COP27 huko Sharm El-Sheikh, Misri, Novemba 8, 2022. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

SHARM EL-SHEIKH, Misri - Nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza ahadi zao za kutoa dola za Kimarekani bilioni 100 katika ufadhili wa tabianchi haraka iwezekanavyo na kuweka mikakati ya kuongeza mara mbili mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi, Mjumbe Maalum wa China kwa Mabadiliko ya Tabianchi Xie Zhenhua amesema Jumanne.

Xie, ambaye pia mwakilishi maalum wa Rais wa China Xi Jinping, ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Utekelezaji wa Hatua za Tabianchi kwenye Mkutano wa 27 (COP27) wa Nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) unaofanyika kwenye mji wa pwani wa Sharm El-Sheikh, nchini Misri.

Amesema kwamba, kukabiliana na changamoto kubwa zinazotokana na hali mbaya ya hewa ya mara kwa mara ambayo imesababisha hasara kubwa katika kila bara na kwa kuibuka kwa migogoro ya nishati na chakula mwaka huu, ushirikiano wa pande nyingi, mshikamano na ushirikiano bado ni njia pekee ya kuondoa tatizo hilo.

“Wakati huo huo, kanuni ya majukumu ya pamoja lakini tofauti na utaratibu wa michango iliyoamuliwa kitaifa bado ni "chaguo lisiloepukika" la kushinda changamoto za tabianchi,” amesema.

Mjumbe huyo wa China amesema, wakati UNFCCC inaadhimisha miaka 30 mwaka huu na Makubaliano ya Paris yameingia katika hatua ya utekelezaji kamili, COP27 inabeba dhamira muhimu ya kushikilia makubaliano juu ya kanuni za UNFCCC na kuhimiza hatua za kivitendo za pande zote.

Akieleza bayana kuwa China imekuwa ikikabiliana kikamilifu na mabadiliko ya tabianchi kwa hatua endelevu na za kivitendo, Xie amesema, kutokana na kuhitimishwa kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), nia ya China ya kufuata njia ya maendeleo ya kijani imeimarishwa zaidi.

"Azimio thabiti na msimamo wa China wa kutekeleza malengo ya kufikia kilele cha kaboni na kufikia usawazishaji wa kaboni, na kushiriki kikamilifu katika udhibiti wa tabianchi duniani hautabadilika kamwe," Xie amesisitiza.

Ameelezea matumaini yake kuwa COP27 itazingatia utekelezaji wa ahadi, huku akizitaka nchi zilizoendelea kuchukua hatua madhubuti katika kupunguza utoaji wa hewa chafu ili kufikia upunguzaji wa hewa ya kaboni kwa kiasi kikubwa kabla ya muda uliopangwa, na kufikia matokeo makubwa katika kujenga uhimilivu na masuala ya ufadhili wa tabianchi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha