Waziri Mkuu wa China awasili Phnom Penh kwa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki, ziara rasmi nchini Cambodia
PHNOM PENH - Kwa mwaliko wa Waziri Mkuu Samdech Techo Hun Sen wa Ufalme wa Cambodia, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amewasili hapa Jumanne jioni kwa ajili ya mikutano mfululizo ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki na ziara rasmi nchini Cambodia.
Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia Hor Namhong na maofisa wengine wakuu wa Cambodia walisalimiana na wajumbe wa msafara wake kwenye uwanja wa ndege. Askari wa gwaride la heshima walijipanga pande zote za zulia jekundu ili kumpa heshima waziri mkuu Li, na vijana walitoa maua kwa Li na mke wake Cheng Hong.
Balozi wa China nchini Cambodia Wang Wentian na Balozi wa China katika Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) Deng Xijun pia wamewakaribisha waziri mkuu Li kwenye uwanja wa ndege.
Li ameweka bayana kuwa China na ASEAN ni washirika wenzi wa kimkakati wa pande zote na washirika wenzi wakubwa zaidi wa biashara.
“Hali ya kimataifa na kikanda inapitia mabadiliko magumu na makubwa, pamoja na kutokuwa na uhakika na utulivu, na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa zinazokabili maendeleo ya kimataifa,” waziri mkuu Li amesema.
Amesema, China inatarajia mikutano ya viongozi wa Asia Mashariki kuangazia maendeleo na ushirikiano, kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, kushikilia ushirikiano wa wazi na kunufaishana, kudumisha kwa pamoja minyororo ya viwanda na ugavi iliyo salama na rahisi duniani, kuwezesha pande husika kushikana mikono kushughulikia changamoto za kimataifa na kuongeza msukumo mpya katika kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda pamoja na kulinda amani, utulivu, maendeleo na ustawi katika kanda na kwingineko.
Amesema China na Cambodia, zikiwa ni majirani wa karibu wenye urafiki wa kitamaduni, zimeendelea kupiga hatua katika ushirikiano wao wa kunufaishana.
“Kupitia ziara hii, China iko tayari kuongeza mshikamano na urafiki wake na Cambodia, kujadiliana kwa pamoja njia ya kusonga mbele kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, na kufanyia kazi matokeo zaidi katika kujenga jumuiya ya China na Kambodia yenye mustakabali wa pamoja ili kutoa manufaa zaidi kwa nchi hizo mbili na watu wake” amesema waziri mkuu Li.
Waziri mkuu Li atahudhuria Mkutano wa 25 wa Wakuu wa China na ASEAN, Mkutano wa 25 wa ASEAN Plus China, Japan na Jamhuri ya Korea na Mkutano wa 17 wa wakuu wa Asia Mashariki utakaofanyika Phnom Penh. Katika ziara yake nchini Cambodia waziri mkuu Li atakutana na viongozi wakuu wa Cambodia na kushuhudia utiwaji saini wa makubaliano mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili.
Mkewe Cheng na Konsela na Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali la China, Xiao Jie pia wanamfuata waziri mkuu Li katika ziara yake hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma