99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kimbunga Ma-on chatua Mkoa wa Guangdong nchini China huku shule, usafiri wa umma ukisimamishwa (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2022
Kimbunga Ma-on chatua Mkoa wa Guangdong nchini China huku shule, usafiri wa umma ukisimamishwa
Katika picha hii iliyopigwa kutoka angani, boti za uvuvi zikiwa zimerejea kwenye bandari kwa ajili ya kuhifadhiwa katika Mji wa Yangjiang, Mkoa wa Guangdong, nchini China, Agosti 24, 2022. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU – Kimbunga Ma-on, ambacho ni kimbunga cha tisa kufika nchini China katika mwaka huu, kimetua kwa kasi ya upepo ya hadi kilomita 118.8 kwa saa, majira ya Saa 4:30 Asubuhi (kwa saa za China) leo Alhamisi kwenye ufukwe wa Mji wa Maoming, katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.

Idara ya Hali ya Hewa ya Mkoa wa Guangdong imesema kuwa, Kimbunga Ma-on kitasonga kuelekea Kaskazini-Magharibi kwa kasi ya takriban kilomita 25 kwa saa, kikipitia mji wa Maoming na kuingia katika Mkoa unaojiendesha wa Guangxi majira ya mchana huku nguvu zake zikidhoofika hatua kwa hatua.

Awali, mkoa huo ulitangaza kufunga shule, maeneo yenye mandhari nzuri, na kutekeleza udhibiti wa usafiri wa barabarani katika baadhi ya maeneo ili kukabiliana na kimbunga hicho.

Idara ya Hali ya Hewa ya mkoa huo imetabiri kutokea kwa mvua kubwa katika maeneo mengi ya Guangdong kuanzia Jumatano jioni hadi Alhamisi.

Shirika la Reli la China, Tawi la Guangzhou pia limetangaza kusimamisha au kupunguza kasi ya uendeshaji wa treni zinazopita katika eneo hilo siku ya Alhamisi.

Ili kuhakikisha usalama wa walimu na wanafunzi, miji kadhaa ya Guangdong imetoa notisi ya kusimamisha masomo.

Makao makuu ya udhibiti wa mafuriko na misaada ya ukame ya Mto Pearl yameboresha jitihada zake za dharura kwa mafuriko hadi Kiwango cha III siku ya Jumatano, ikiwa ni mwitikio wa tatu kwa ukali zaidi katika mfumo wa kukabiliana na dharura wenye ngazi nne wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha