99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

WHO yasema DRC imeripoti kisa kimoja kinachoshukiwa kuwa cha Ebola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2022
WHO yasema DRC imeripoti kisa kimoja kinachoshukiwa kuwa cha Ebola
Picha hii kutoka maktaba iliyopigwa Tarehe 21 Machi 2021, ikionyesha mhudumu wa afya akinyunyizia dawa za kuua vijidudu kwenye kituo cha matibabu cha Ebola katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Picha na Alain Uaykani/Xinhua)

BRAZZAVILLE - Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika limesema kupitia taarifa yake ya Jumamosi kwamba, Mamlaka ya afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inachunguza kisa kinachoshukiwa kuwa cha maambukizi ya virusi vya Ebola, katika Jimbo la Kivu Kaskazini, Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo, wakati ambapo mlipuko wa hivi punde wa Ebola nchini DRC ulitangazwa kumalizika mapema Julai.

“Kisa hicho kinachoshukiwa ni cha mwanamke mwenye umri wa miaka 46 aliyefariki Agosti 15 huko Beni, Mji wa Kivu Kaskazini. Mgonjwa huyo awali alipata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Beni, kwa ajili ya magonjwa mengine, lakini baadaye, alionyesha dalili zinazofanana na ugonjwa wa Ebola,” inasema taarifa hiyo ya WHO na kubainisha kuwa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ya DRC (INRB) inaendelea na uchunguzi wa sampuli kutoka kwa mgonjwa huyo ili kuamua ikiwa mgonjwa aliambukizwa Ebola.

"Wakati uchambuzi ukiendelea, WHO iko tayari kusaidia maafisa wa afya kuchunguza kisa hicho na kujiandaa kwa uwezekano wa kuzuka," Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika amesema.

Julai 4, DRC ilitangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa hivi punde wa Ebola uliolipuka chini ya miezi mitatu iliyopita huko Mbandaka, Mji Mkuu wa Jimbo la Equateur, Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo. Kulikuwa na visa vinne vilivyothibitishwa na kisa kimoja kinachodhaniwa, ambapo wote walifariki. Huu ulikuwa milipuko ya tatu katika jimbo hilo tangu Mwaka 2018 na wa 14 kwa ujumla katika nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha