99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wachina nchini Uganda watoa msaada wa chakula kwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo linalokumbwa na njaa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2022
Wachina nchini Uganda watoa msaada wa chakula kwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo linalokumbwa na njaa
Watu wakipakua vitu vya kuokoa maafa kutoka lori kwenye hafla ya kukabidhiana vitu iliyofanyika Kampala, Uganda Agosti 19, 2022. (Picha/Xinhua)

Wachina wanaokaa nchini Uganda wametoa tani 20 ya msaada wa chakula kwa watu wanaoathiriwa na njaa kwenye Kaskazini Mashariki mwa Uganda.

Shirikisho la Fuqing la China nchini Uganda pamoja na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China Ijumaa ya wiki iliyopita zilikabidhi msaada huo wa chakula kwa ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia mambo ya kibinadamu.

Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja alisema kwenye taarifa iliyotolewa Ijumaa ya wiki iliyopita kuwa, msaada huo wa chakula utachangia juhudi za nchi hiyo za kupunguza athari ya ukame uliotokea kwenye eneo la Karamoja.

“Nikiwa kwa niaba ya serikali ya Uganda nawashukuru marafiki zetu wa China kwa msaada waliotoa wa tani 20 za unga wa mahindi, maharage, chumvi na mafuta ya kupika kwa ajili ya wazee wa Karamoja wenye hali ya udhaifu,” alisema Bi.Nabbanja. “Hizi ni nyongeza zinazokaribishwa kwa juhudi zetu za kuwasaidia watu wenye mahitaji .”

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Uganda lilitoa wito wa kutoa msaada Mwezi Juni, kwa kuwa kuna watu zaidi ya 500,000 wanaokumbwa na njaa kwenye eneo la Kaskazini Mashariki, ambapo hali ya nusu ukame inaonekana huko. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha