Maonesho ya michezo ya sanaa ya watoto wanaoishi sehemu ya milimani (7)
![]() |
Agosti 20, watoto wakionesha mchezo wa sanaa. |
Kituo cha Mawasiliano ya michezo ya sanaa na utamaduni cha Dayuanshe katika Kijiji cha Dayuanziran cha Mji wa Shuishi wa Wilaya ya Ningyuan ya Mkoa wa Hunan kilianzishwa mwaka 2016 na vijana wawili waliorudi kijijini kufanya kazi baada ya kuhitimu chuo kikuu cha uchoraji, ambao waliona vijinini humo kulikuwa na watoto wengi ambao wazazi wao wanafanya kazi nje ya vijiji, hivyo walitaka kuwasaidia watoto hao kupata mafunzo ya Sanaa na kuwawezesha waone mambo mbalimbali duniani ili kukua vizuri zaidi.
Miaka sita baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha Dayuanshe, kumekuwa na watoto zaidi ya 3000 ambao wameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za maonesho ya michezo ya sanaa za kituo hicho. Mbali na walimu kadhaa walioko huko ambao hutumia nafasi za jioni na wikendi kufundisha watoto, wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya sehemu mbalimbali huja kufundisha wanafunzi kila likizo ya majira ya baridi na majira ya joto.
Mwezi Julai wa mwaka huu, watoto zaidi ya 70 waliotoka vijiji na miji midogo iliyoko karibu na kituo hicho walishiriki kwenye shughuli ya majira ya joto ya Kituo cha Dayuanshe, ambapo walisoma masomo ya sanaa ya mikono, uchoraji wa picha na muziki baada ya kumaliza masomo yao shuleni. Jioni ya tarehe 20, maonesho ya michezo ya sanaa yaliyoandaliwa pamoja na watoto na wanavijiji ilikuwa kama “sherehe ya kuhitimu”. Watoto walitunga michezo yao ya Sanaa na kusanifu mavazi wao wenyewe , watoto zaidi ya 40 waliovaa mavazi yao wakisubiri kufanya maonesho yao ya michezo ya sanaa vijijini.
(Mpiga picha: Chen Zhenhai/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma