Xi’an: kusukuma mbele uchumi wa wakati wa usiku na kutoa uwezo wa matumizi
Siku za hivi karibuni, Mji wa Xi’an ulitoa hatua kadhaa za kuendeleza kwa nguvu kubwa shughuli za kiuchumi nje ya majengo na wakati wa usiku ili kuonesha nguvu ya matumizi ya watu.
Hatua ya kwanza ni kuruhusu makampuni makubwa ya biashara yatumie viwanja vilivyoko mbele ya maduka yao kukuza biashara kwa utaratibu; pili ni kuongoza, kuhimiza na kuunga mkono makampuni kuanzisha mfumo mpya wa matumizi kama vile vya kuanzisha magulio ya mada ya mapumziko na burudani; tatu ni kuunga mkono makampuni ya uuzaji wa magari na vyombo vya umeme nyumbani kuingia kwenye uwanja, makazi na vijiji kufanya shughuli za kukuza uuzaji; nne ni kuunga mkono kutumia sehemu za umma za mijini kufanya shuguli za kukuza uuzaji zenye mada maalum; tano ni kuruhusu mitaa ya biashara yenye mazingira yanayofaa kufunguliwa kwa mabanda yao ya biashara wakati wa usiku na kuongeza muda wa kufunguliwa wakati wa usiku; sita ni kuanzisha shughuli za aina mpya za matumizi ya wakati wa usiku, kutegemea maeneo maalum ya mitaa ya biashara kufanya shughuli nje kama kuweka magulio ya bidhaa za kiutamaduni na kutembelea wakati wa usiku mjini Xi’an, ili kuendeleza shughuli za uchumi wakati wa usiku na kuonesha nguvu yake ya uhai.
(Mpiga picha: Liu Xiao/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma