99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Namibia yatarajia kupokea watalii wa kimataifa zaidi ya 500,000 katika Mwaka 2022 (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2022
Namibia yatarajia kupokea watalii wa kimataifa zaidi ya 500,000 katika Mwaka 2022
Watalii wakipiga picha kwenye ufukwe wa bahari huko Swakopmund, Namibia, Mei 26, 2022. (Xinhua/Chen Cheng)

WINDHOEK - Waziri wa Mazingira wa Namibia, Pohamba Shifeta Alhamisi wiki hii katika taarifa yake amesema kwamba, nchi hiyo inatarajia kupokea watalii wa kimataifa zaidi ya 500,000 katika Mwaka 2022, kutoka watalii 354,508 waliotembelea nchi hiyo Mwaka 2021.

Shifeta amesema janga la UVIKO-19 limeipa Namibia fursa ya kuboresha mfumo wezeshi wa kuanzisha upya sekta hiyo.

“Namibia itazindua programu lengwa za kuingilia kati katika sekta ya utalii kupitia utayarishaji na utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kufufua Utalii wa Mwaka 2022 hadi 2024” amesema.

"Mpango umebainisha sera muhimu, programu za kimkakati na shughuli zinazohitajika ili kurejesha sekta hiyo kuwa na yenye nguvu na bora zaidi," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha