Hospitali ya kwanza ya muda ya mchemraba yaanza kufanya kazi mjini Changchun (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2022
![]() |
Hospitali ya muda ya mchemraba katika Kituo cha Mikutano na Maonesho cha Kimataifa cha Changchun,China imeanza kufanya kazi jana. (Mpiga picha: Zhang Yang) |
Machi 15, Hospitali ya kwanza ya muda ya mchemraba iliyojengwa katika Kituo cha Mikutano na Maonesho cha Kimataifa cha Changchun, China, ilifunguliwa rasmi, na usiku wa siku hiyo ilianza kupokea na kutibu wagonjwa wasioonekana dalili au wenye dalili kidogo za kuambukizwa virusi vya korona. Hivi sasa, kumbi namba 2, 3, 4 na 5 za hospitali hiyo ya muda ya mchemraba zimekamilika na vitanda 1500 vimeanza kutumiwa. Kumbi namba 8 na 9 zitakamilika hivi karibuni, ambapo vitawekwa vitanda 750. Hospitali kuu ya Mji wa Changchun imeanza kufanya uendeshaji wa hospitali hiyo ya muda ya mchemraba na imetuma madaktari na wafanyakazi karibu 100.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma