

Lugha Nyingine
Bondia wa Kike wa Tanzania apania kuvunja upendeleo wa kijinsia kwa ngumi zake
![]() |
Bondia wa kike wa Tanzania Pendo Njau akiwa katika picha pamoja na mabondia wengine huko Dar es Salaam, Tanzania Machi 4, 2022. (Herman Emmanuel/Xinhua) |
“Maoni yote yanayohusu upendeleo wa kijinsia yanaweza kuvunjwa kwa kutumia ngumi zenye nguvu kama zangu,” anasema Hellen Honest Njau, ambaye pia hujulikana kama Pendo Njau.
Njau, ambaye pia ni mama wa watoto watatu, ni bondia na mwamuzi wa michezo ya masumbwi au ndondi huko Dar es Salaam, Tanzania.
“Jasho ni mojawapo ya vipodozi vyangu,” Njau huku akitabasamu anajibu swali la Shirika la Habari la China, Xinhua kabla ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha mafanikio ya kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa ya wanawake inayokumbukwa Machi 8 kila mwaka.
Njau ni mwanachama wa Kamisheni ya Udhibiti wa Michezo ya Masumbwi ya Kulipwa ya Tanzania (TPBRC), ambayo inaidhinisha leseni, kudhibiti na kusimamia michezo ya masumbwi ya kulipwa nchini Tanzania.
Kwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Njau ana ujumbe mmoja kwa wasichana: “Wazazi au walezi wanatakiwa kuwaruhusu watoto wao wa kike kushiriki katika kazi za uzalishaji kama vile masumbwi, ambazo zitawawezesha wapate kipato kwa ajili ya kusaidia familia zao katika siku za baadaye.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma