99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Msaada wa Masanduku 150,000 ya Dawa za Mitishamba kutoka China Bara wafika Hong Kong (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2022
Msaada wa Masanduku 150,000 ya Dawa za Mitishamba kutoka China Bara wafika Hong Kong
Edward Yau (wa nne kutoka kushoto), Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi wa Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), akiwa katika picha ya pamoja na wahusika wengine wakati wa kufika kwa shehena ya kwanza ya masanduku 150,000 ya dawa za mitishamba za China (TCM) za kutibu UVIKO-19 zilizotolewa na China Bara, ikiwa pamoja na mahitaji mengine yaliyoagizwa ya kukabiliana dhidi ya maambukizi huko Kusini mwa China Hong Kong, Februari 20, 2022. Masanduku zaidi ya 300,000 ya TCM za aina mbalimbali yatasafirishwa kutoka China Bara mpaka Hong Kong kwa makundi. Shehena ya kwanza ya barakoa KN95 milioni 25 iliyotolewa na China Bara pia imefika kwa makundi hivi karibuni. (Xinhua/Li Gang)

Shehena ya kwanza ya masanduku 150,000 ya dawa za mitishamba za China (TCM) za kutibu UVIKO-19, pamoja na mahitaji mengine yanayohitajika katika kujikinga dhidi ya virusi vya korona yaliyotolewa msaada na China Bara yamefika Hong Kong Jumapili ya wiki iliyopita.

“Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) inashukuru Serikali Kuu kwa kujali wakazi wa Hong Kong na kuunga mkono kazi ya kujikinga dhidi ya virusi vya korona ya Hong Kong,” alisema Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi Edward Yau, ambaye pia anaongoza kikundi cha kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya matibabu, ikiwemo kuratibu misaada ya matibabu kutoka China Bara mpaka Hong Kong.

Ili kuongeza uwezo wa “kuthibitisha mapema, kutenga mapema, kutibu mapema” watu waliokutwa na maambukizi, Serikali ya HKSAR inajitahidi kununua vifaa vya RAT zaidi ya milioni 100, ambavyo vitaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Hong Kong wa kupima kwa haraka. Vifaa hivyo vitagawiwa kwanza kwa watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa na makundi lengwa ya watu. Kuanzia Februari 19, shehena ya kwanza ya vifaa vya RAT milioni 10 iliyotolewa na China Bara imefika Hong Kong kwa makundi tofauti tangu Februari 19.

Licha ya hayo, masanduku zaidi ya laki tatu (300,000) ya TCM za aina mbalimbali yatasafirishwa kutoka China Bara mpaka Hong Kong kwa makundi tofauti. Shehena ya kwanza ya barakoa za KN95 milioni 25 zilizotolewa na China Bara pia imefika huko kwa makundi katika siku chache zilizopita.

Wakati huo huo, takwimu kutoka serikalini zinaonesha kuwa, Hong Kong Jumapili ya wiki iliyopita iliripoti wagonjwa wapya 6,067 wa UVIKO-19 katika saa 24 zilizopita katika mkoa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha