99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mpangilio wa maonesho ya nne ya CIIE waanza huku bidhaa zitakazooneshwa zikiwasili (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2021
Mpangilio wa maonesho ya nne ya CIIE waanza huku bidhaa zitakazooneshwa zikiwasili
Kituo cha Kitaifa cha Maonesho na Mikutano, Shanghai, Kituo Kikuu cha Maonesho ya nne ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) (Tovuti ya Gazeti la Umma/Ji Haixin)

Shehena ya kwanza ya bidhaa zitakazooneshwa katika Maonesho ya nne ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) imeingia katika Kituo cha Kitaifa cha Maonesho na Mikutano cha Shanghai asubuhi ya Oktoba 23, kuashiria kuanzishwa kwa kazi ya kuandaa mabanda ya maonesho hayo.

Mashine hizo zilizowasili ni pamoja na mashine ya kupinda kutoka kampuni ya Amada ya Japan pamoja na lori la forklift na trekta ya umeme iliyoletwa na kampuni ya Ujerumani Jungheinrich AG.

Hadi kufikia Tarehe 23, Oktoba mwaka huu, shehena 150 za bidhaa na vifaa vitakavyooneshwa kwenye maonesho ya nne ya CIIE zilikuwa zimeshaingizwa nchini China kupitia Bandari za Shanghai, ikiwa inamaanisha kwamba zaidi ya asilimia 98 ya bidhaa na vifaa vitakavyooneshwa kwenye maonesho hayo vimeshaingia China.

Maeneo yote ya maonesho ya CIIE yataanza kujenga vibanda na kupanga bidhaa na vifaa vitakavyooneshwa. Kazi nzima ya maandalizi inatarajiwa kukamilika karibu Novemba 2.

Jumla ya eneo zima la Maonesho ya nne CIIE inazidi mita za mraba 360,000, na idadi ya kampuni ya biashara pamoja na nchi na kanda zinazotarajiwa kushiriki maonesho ya mwaka huu inazidi maonesho ya tatu ya CIIE yaliyofanyika mwaka jana, Xue Feng, Mkurugenzi wa Mambo ya Kigeni wa Bodi ya Maendeleo ya Uwekezaji ya Shanghai amesema na kuongeza kuwa kampuni zilizo katika orodha ya Kampuni Bora 500 duniani, na kampuni nyigine kubwa zimejiandikisha kushiriki kikamilifu maonesho yajayo, huku zaidi ya asilimia 80 ya kampuni zilizoshiriki maonesho ya mwaka jana zikiendelea kushiriki tena mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ma Fengmin, Mkurugenzi wa idara ya fedha ya CIIE, maonesho ya nne ya CIIE ya mwaka huu yatajumuisha maonyesho ya nchi, maonyesho ya kampuni na biashara na Kongamano ya nne ya Kiuchumi ya Kimataifa ya Hongqiao.

Takriban nchi 60 zimethibitisha kushiriki katika maonesho ya nchi ya mtandaoni, ambayo yalizinduliwa kwa majaribio Tarehe 13 Oktoba. Maonesho ya biashara katika maonyesho ya nne ya CIIE, ambayo yanajumuisha maeneo sita makubwa ya maonesho, yanatarajiwa kushirikisha karibu kampuni 3,000 kutoka zaidi ya nchi na sehemu 120, ambazo nyingi zitazindua bidhaa zao mpya, teknolojia na huduma mpya kwenye maonyesho hayo.

Kwa mara ya kwanza, maonesho hayo yameruhusu waoneshaji na mashirika husika kuwaalika wateja wao kuwa wageni wa kitaalamu wa CIIE.

Jumla ya vikundi 39 vya kibiashara na vikundi vidogo vipatavyo 600 vimejipanga kushiriki maonesho hayo. Zaidi ya wanunuzi 2,700 walishiriki katika shughuli 18 za maonesho ya mtandaoni na nje ya mtandao, na zaidi ya waoneshaji 200 wamesaini mikataba na wanunuzi zaidi 500 wakati wa mikutano ya awali ya kukutanisha wauazaji na wanunuzi wa bidhaa.

Hadi sasa, watu 310,000 kutoka taasisi 90,000 wamejisajili kushiriki katika maonesho haya ya nne ya CIIE.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha