99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais wa China ahutubia maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa vita dhidi ya uvamizi wa Japan

(CRI Online) Septemba 03, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais wa China Xi Jinping amehutubia mkutano mkubwa wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na ushindi wa Dunia wa Vita vya Kupinga Ufashisti uliofanyika katika Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing.

Katika hotuba yake, rais Xi amesema ustawishaji wa taifa la China hauwezi kuzuiliwa, na vita kubwa na ngumu ya kupambana na uvamizi, imeonesha ushindi kamili wa kwanza wa China dhidi ya uvamizi kutoka nje katika zama za sasa.

Rais Xi amesema, ushindi wa vita hivyo ulipatikana chini ya bendera ya umoja wa kitaifa wa kupambana na uvamizi wa Japan ulioanzishwa kwa utetezi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na kwamba watu wa China wametoa mchango mkubwa katika uokoaji wa ustaarabu wa binadamu na kulinda amani ya dunia kwa kujitolea katika vita, ambayo ni sehemu muhimu sana ya vita vya dunia vya kupinga Ufashisti.

Amesema ni pale tu mataifa duniani yatakapotendeana kwa usawa, kuishi kwa masikilizano na kuungana mkono ndipo usalama wa pamoja utalindwa, chanzo cha vita kuondolewa, na majanga ya kihistoria kuzuiwa kutokea tena.

Katika hotuba hiyo, rais Xi pia amesema katika zama za sasa, binadamu anakabiliwa na uamuzi wa kuwa na amani ama vita, majadiliano au makabiliano, na matokeo ya ushindi wa pamoja ama mchezo usio na matokeo yoyote.

Amesema watu wa China watasimama kithabiti katika upande sahihi wa historia na upande wa maendeleo ya binadamu, kushikilia kufuata njia ya maendeleo kwa amani, na kushikana mkono na dunia ili kujenga jumuiya ye binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Ametoa wito wa kuwataka watu wa makabila yote wa China kuwa na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii chini ya uongozi thabiti wa CPC ili kujenga nchi yenye nguvu na kuendeleza ustawishaji wa taifa katika sekta zote kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi amelitaka Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kutoa uungaji mkono wa kimkakati kwa ustawishaji wa taifa na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

Pia amelitaka Jeshi hilo kujijenga na kuwa jeshi la kiwango cha juu duniani na kulinda kithabiti mamlaka ya nchi, muungano na ukamilifu wa ardhi.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha