

Lugha Nyingine
Marais wa China na Russia wafanya mazungumzo
(Picha/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China Jumanne amefanya mazungumzo na rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye yupo ziarani nchini China kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) wa mwaka 2025, na Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa vita vya watu wa China dhidi ya uvamizi ya Japan na ushindi wa vita vya dunia vya kupinga ufashisti.
Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa China na Russia zina msukumo mkubwa wa kujiendeleza, na kwamba zinatakiwa kuongeza uthabiti wa ushirikiano na kuimarisha na kulinda hali ya jumla ya ushirikiano.
Kwa upande wake rais Putin amesema Russia iko tayari kudumisha ushirikiano wa kimkakati na China, kuimarisha mawasiliano ya viongozi wa ngazi ya juu na kuongeza ushirikiano wa kiutendaji katika sekta mbalimbali, ili kukuza maendeleo ya kiwango cha juu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma