99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Xi aongoza Mkutano wa Saba wa Wakuu wa China, Russia na Mongolia

(CRI Online) Septemba 03, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping, pamoja na wenzake wa Russia Vladimir Putin na Mongolia Ukhnaa Khurelsukh, wamefanya mkutano wa saba wa wakuu wa nchi hizo tatu asubuhi ya tarehe 2 Septemba, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Xi Jinping alisema kwamba katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano wa pande tatu kati ya China, Russia na Mongolia umeimarika na kupata matunda yanayoonekana. Mpango wa kipindi cha katikati wa ushirikiano wa pande tatu umetekelezwa kwa mafanikio, biashara kati ya nchi tatu imeongezeka kwa kasi, na ushirikiano katika uchumi, biashara, sayansi na teknolojia, ulinzi wa ikolojia, na mawasiliano kati ya watu na watu umeendelea kuongezeka. Zikiwa nchi jirani marafiki waliounganishwa na milima na mito na kushuhudia kwa pamoja mafanikio na taabu, China inapenda kushirikiana na Russia na Mongolia katika kudumisha dhamira ya awali ya ushirikiano, kujiepusha na uingiliaji kati kutoka nje, na kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya hali ya juu ya ushirikiano wa pande tatu.

Xi Jinping alitoa mapendekezo matatu ya kukuza ushirikiano kati ya China na Russia na Mongolia, yaani kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuimarisha ushirikiano ndani ya utaratibu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO.

Kwa upande wake, rais Putin alisema kuwa Russia, China na Mongolia ni majirani wema na wenye desturi ya muda mrefu ya ushirikiano. Kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa ni muhimu na kutasaidia kuimarisha msingi wa uhusiano wa pande tatu.

Naye rais Khurelsukh alisema kuwa China na Russia ni majirani muhimu wa Mongolia. Mongolia imejizatiti katika kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili, kupanua ushirikiano wa pande tatu, kuendeleza ujenzi wa Ushoroba wa Kiuchumi wa China-Mongolia-Russia, na kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo tatu na kuhimiza maendeleo na ustawi wa kikanda. Ameongeza kuwa mwaka huu ni kumbukizi ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita Vikuu vya Kulinda Nchi vya Umoja wa Kisovieti. Watu wa Mongolia, China na Russia wanapaswa kusherehekea na kuadhimisha kwa pamoja wakati huu wa kihistoria na kukuza mtazamo sahihi wa historia ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha