

Lugha Nyingine
Miaka 20 ya wazo la “milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha”: Teknolojia ya nishati ya jua ya China inayohimiza mustakabali wa nishati ya kijani duniani
Jua linachomoza kwenye mlima wa mashariki wa Milima Tianshan. Zaidi ya paneli za jua (heliostati) 14,500 zilizopangwa katika miduara kuzunguka mnara wa kati unaofyonza joto, huzunguka kama alizeti, zikilenga mwanga wa jua na joto. Huu ni utaratibu wa kila siku wa "kufuata jua" wa kituo cha kuzalisha megawati 50 za umeme wa nishati ya jua cha mnara wa chumvi iliyoyeyushwa huko Hami mkoani Xinjiang.
Jua linazama kwenye mkoa wa Cape kaskazini nchini Afrika Kusini. Paneli za nishati ya jua zinarudi polepole kwenye nafasi zao, na chumvi iliyoyeyushwa yenye nyuzi joto 565 iliyohifadhiwa mchana inaendelea kutoa joto, na hivyo kuhakikisha uwepo endelevu wa umeme kwa saa 24. Hiki ni kituo cha kwanza barani Afrika cha kuzalisha megawati 100 za umeme wa nishati ya jua kwa kutumia chumvi iliyoyeyshwa, kilichojengwa kwa ushirikiano na makampuni ya China, ambacho kinaweka kigezo kipya cha ushirikiano wa nishati ya kijani kati ya China na Afrika.
Kuunda muujiza wa kuzalisha nishati ya kijani katika Jangwa kubwa la Gobi, ni mfano wazi wa kuchangia busara za China na uzoefu wa kutekeleza mpango kwa maendeleo endelevu duniani.
Katibu Mkuu Xi Jinping alisema, “Kusimamia uhusiano kati ya maendeleo na ulinzi wa mazingira ni changamoto ya kimataifa, na ni somo la milele linaloyakabili maendeleo ya binadamu.” Mwaka huu ni miaka 20 ya kutolewa kwa wazo la “Milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha.” Uzoefu wa usimamizi wa mazingira ya asili wa China, ukiongozwa na fikra ya ustaarabu wa ikolojia ya Xi Jinping, umepanda mbegu za maendeleo ya kijani duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma