99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Soko la Xicang lenye historia ya Miaka 100 Mjini Xi'an, China lajaa hali moto moto ya manunuzi (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2025
Soko la Xicang lenye historia ya Miaka 100 Mjini Xi'an, China lajaa hali moto moto ya manunuzi
Watalii wakinunua bidhaa kwenye Soko la Xicang katika Eneo la Lianhu la Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Julai 5, 2025. (Xinhua/Zou Jingyi)

Soko la Xicang katika Eneo la Lianhu la Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China hapo awali lilikuwa sehemu ya ghala la nafaka la China wakati wa Enzi za Ming na Qing ya nchi hiyo ya zama za kale, na sasa hujaa hali moto moto ya maisha kila Alhamisi na Jumapili. Gulio hilo lenye historia ya miaka 100 limepitia hali mbalimbali na kuwa moja ya vituo vikubwa zaidi vya biashara ya mitumba vya ngazi ya chini, vilevile ni alama hai ya mila na desturi za jadi za wenyeji.

Tangu mwaka 2024, maeneo hayo yamekuwa yakipitia juhudi za kuhuisha miji ili kusaidia kuhifadhi soko hilo la jadi katika msingi wake wakati huohuo kuboresha miundombinu iliyopo, na kujenga upya Bustani ya Kumbukumbu za Mji ya Xicang. Mkakati huo umeruhusu mitindo ya kisasa ya vijana kuishi pamoja na mvuto wa kipekee wa soko, ikiingiza hali mpya moto moto kwenye eneo hilo la kihistoria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha