99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Dhoruba ya mvua yawalazimisha wakaazi zaidi 3,000 kuhama katika maeneo ya vitongoji vya Beijing, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2025
Dhoruba ya mvua yawalazimisha wakaazi zaidi 3,000 kuhama katika maeneo ya vitongoji vya Beijing, China
Waokoaji wakisafisha daraja lililozibwa katika Kijiji cha Xiwanzi cha Tarafa ya Shicheng, Eneo la Miyun la Beijing, mji mkuu wa China, Julai 27, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Mvua kubwa imesababisha wakaazi zaidi ya 3,000 kuhama katika eneo la Miyun, Mji wa Beijing, Mji Mkuu wa China ambapo idara ya hali ya hewa katika eneo hilo ilitoa tahadhari nyekundu juu ya mvua kubwa saa 3:06 usiku wa Jumamosi, kiwango cha juu zaidi katika mfumo wa tahadhari ya hali ya hewa wa ngazi nne wa China wenye alama za rangi.

Kati ya saa 6 mchana Jumamosi na saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili, eneo hilo lilirekodi wastani wa mvua wa milimita 73.5, huku mvua kubwa zaidi ikifikia milimita 315.3 katika Kituo cha Huangtuliang.

Makao makuu ya udhibiti wa mafuriko na misaada ya ukame ya Miyun yamepandisha mwitikio wa dharura wa kudhibiti mafuriko wa Ngazi ya I ili kutekeleza shughuli husika za uokoaji.

Hali mbaya ya hewa ililazimisha kufungwa kwa barabara kuu 12 katika eneo la Miyun, saba kati ya hizo zimeshafunguliwa tena. Mawasiliano na vijiji vyote vilivyoathiriwa yamepatikana, na jumla ya wakazi 3,065 katika vijiji 149 wamehamishwa salama hadi kufikia saa 11 alfajiri siku ya Jumapili.

Hakuna vifo vilivyoripotiwa -- wakati huohuo shughuli za uhamishaji na uokoaji watu bado zinaendelea.

Katika mji wote wa Beijing, njia 88 za mabasi, zinazohudumia maeneo ya vitongoji, zimetekeleza marekebisho ya dharura – ikiwemo kusimamishwa kwa huduma, kufupisha na kubadili njia, kamati ya usafiri ya mji huo imesema.

Pia, shughuli za treni kwenye njia tatu za reli na huduma za usafiri wa majini katika maeneo ya Miyun, Huairou na Yanqing zimesitishwa -- huku boti zote za watalii na feri zikiamriwa kubaki kwenye gati.

Maeneo mengi ya Beijing yalikuwa yakitabiriwa kupata mvua inayozidi milimita 30 kwa saa kati ya Jumapili alasiri na Jumatatu asubuhi, amesema mtaalamu mkuu wa hali ya hewa Zhang Linna kutoka idara ya hali ya hewa ya Beijing.

Zhang ameongeza kuwa maeneo kadhaa, yakiwemo Yanqing, Huairou, Miyun na Pinggu, huenda yakashuhudia mvua ikizidi milimita 50 kwa saa, na jumla ya mvua katika baadhi ya maeneo huenda ikazidi milimita 100.

Utabiri huo unaonyesha hatari kubwa zaidi za majanga ya mara ya pili katika maeneo ya milima na chini ya milima – yakiwemo ya mafuriko, maporomoko ya udongo na maporomoko ya ardhi. Maeneo ya ukanda wa chini yanakabiliwa na hatari kubwa ya mafuriko, inayohitaji umakini mkubwa na hatua za kuzuia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha