

Lugha Nyingine
Watalii wanaoingia China kutoka nje wazama katika wimbi la manunuzi mjini Shanghai
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2025
China sasa inatoa msamaha wa viza wa upande mmoja kwa nchi 47 na msamaha wa visa kwa wasafiri wa nchi 55 wanaoingia China kuunganisha ndege kwenda nchi nyingine, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning alisema Julai 11.
Kwa kuchochewa na sheria hizo za viza zilizolegezwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wamiliki wa pasipoti za kigeni wanaoingia China, ikisababisha kuongezeka kwa matumizi ya watalii wanaoingia China kutoka nje.
Ukiwa umejiweka katika nafasi ya kuwa kituo cha utalii cha ngazi ya kimataifa chenye mvuto duniani, Mji wa Shanghai ulioko mashariki mwa China umeshuhudia matumizi makubwa ya watalii wanaoingia China kutoka nje katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma