

Lugha Nyingine
China yainua kiwango cha kukabiliana na hali ya dharura ya Kimbunga Wipha katika mikoa ya Guangdong na Hainan
![]() |
Magari yakiendeshwa kupita eneo lililofurika maji mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Julai 20, 2025. (Xinhua/Yang Guanyu) |
BEIJING - Makao Makuu ya Mafuriko na Kupambana na Ukame ya China yameinua kiwango cha kukabiliana na hali ya dharura ya mafuriko na kimbunga hadi ngazi ya III kwenye mikoa ya kusini mwa China ya Guangdong na Hainan katika mwitikio wa Kimbunga Wipha na kudumisha Ngazi ya IV ya kupambana na hali ya dharura ya kimbunga katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi.
Kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, Kimbunga Wipha kilikuwa kinatabiriwa kuleta dhoruba na mvua kubwa katika baadhi ya sehemu mikoani Hainan na Guangdong kuanzia jana Jumapili hadi leo Jumatatu.
Wakati huohuo, shehena za msaada wa mahitaji zilikuwa zimepelekwa kwa Guangdong na Hainan na ofisi ya kamati ya kitaifa ya kuzuia, kupunguza na kutoa msaada kwa kukabiliana na maafa, Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China, na Idara ya Kitaifa ya Hifadhi za Chakula na za Kimkakati ya China. Mahitaji hayo yakiwemo vitu 33,000 pamoja na vitanda vya kukunjwa, mifarishi na taa.
China imekuwa na mfumo wa kupambana na hali ya dharura wa ngazi nne, kati yao Ngazi ya I ikiwa ni ya dharura zaidi na usimamizi mkali zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma