99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Serengeti, Zanzibar, Kilimanjaro miongoni mwa vivutio vya utalii vya Tanzania washindi katika Tuzo za Utalii Duniani

(CRI Online) Juni 30, 2025

Tanzania imeibuka kinara wa utalii wa Afrika kwenye Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards 2025), zilizofanyika Jumamosi mjini Dar es Salaam.

Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania imesema Tanzania si tu imekuwa mwenyeji wa hafla ya mwaka huu ya utoaji tuzo hizo, lakini pia imeweka historia na kufanikiwa kuvunja rekodi kwa kupata tuzo 27 kuhusu mandhari yake ya kuvutia, sekta ya huduma za utalii, na taasisi za kipekee za utalii.

Miongoni mwa tuzo hizo ni pamoja na zile za eneo linalovutia zaidi kwa utalii, bodi ya utalii inayoongoza, na mbuga ya wanyama inayoongoza.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii ya Tanzania inaonesha kuwa vivutio vya kitalii vilivyotambuliwa katika tuzo hizo ni Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, fukwe safi za Zanzibar na Hifadhi ya Taifa ya Kitulo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha