99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ethiopia yatangaza kufungua sekta ya benki kwa benki za kigeni

(CRI Online) Juni 27, 2025

Benki Kuu ya Ethiopia imetangaza kwamba, kwa mara ya kwanza, sekta ya benki nchini humo iko wazi kwa benki za kigeni na wawekezaji, ikiwaruhusu kushiriki katika biashara ya benki nchini humo kwa kuanzisha kampuni tanzu, matawi au ofisi za uwakilishi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano wiki hii na Benki hiyo, kuanzia siku hiyo, benki na wawekezaji wa kigeni wanaweza kutuma maombi ya leseni za benki kwa Benki Kuu ya Ethiopia.

Taarifa hiyo pia imesema Benki hiyo inatumai hatua hiyo italeta uwekezaji zaidi na ushindani kwa Ethiopia na kusaidia kuboresha kiwango cha huduma, ufanisi na ujumuishaji wa sekta ya benki nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha