99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yasema kitendo cha kishujaa cha daktari wa China nchini Tanzania kimeonyesha urafiki wa kina kati ya China na Afrika

(CRI Online) Juni 25, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesema, kitendo cha kishujaa cha daktari Zhang Junqiao wa China ambaye alijitoa mhanga maisha yake kuokoa mtu aliyekuwa akizama baharini nchini Tanzania kimeonyesha vitendo halisi kwa urafiki wa kina kati ya China na Afrika, na moyo wa kujitolea, mapenzi na nia ya dhati ya timu ya madaktari wa China katika kuokoa uhai wa watu.

Akijibu swali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne mjini Beijing, Guo ametumia fursa hiyo pia kutoa pole kwa familia ya Zhang, akisema kuwa inasikitisha kupoteza mjumbe muhimu wa timu za madaktari wa China barani Afrika.

Zhang Junqiao, alikuwa ni kiongozi wa timu ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania na mtaalamu wa ganzi, ambaye alifariki dunia tarehe 15 mwezi huu wakati akimwokoa mwanamke aliyekuwa akizama katika pwani ya jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Guo amesema, wajumbe wa timu za madaktari wa China wamekuwa wakitibu na kuokoa maisha ya wenyeji, na kutoa mafunzo kwa timu za madaktari katika nchi husika, huku akiongeza kuwa, kazi ya timu za madaktari zimechangia sana katika urafiki kati ya China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha