99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia?na China

(CRI Online) Juni 12, 2025

Rais Xi Jinping wa China kwenye barua aliyoituma Jumanne kutoa salamu za pongezi kwa Mkutano wa Mawaziri Waratibu wa Utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ametangaza kuwa China itasamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China.

“China iko tayari kujadiliana na kutia saini makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya China na Afrika kwa Maendeleo ya Pamoja ili kutekeleza utozaji ushuru sifuri kwa asilimia 100 ya viwango vya ushuru kwa nchi 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China,” Rais Xi amesema, akiongeza kuwa China itatoa urahisi zaidi kwa nchi zenye maendeleo madogo zaidi barani Afrika kusafirisha kuuza bidhaa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha