99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Shughuli za utalii nchini China zaongezeka kwa 5.7%?wakati wa mapumziko ya Sikukuu ya Duanwu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2025
Shughuli za utalii nchini China zaongezeka kwa 5.7%?wakati wa mapumziko ya Sikukuu ya Duanwu
Watalii wakitembelea eneo la mtaa wa kale wa Hetou mjini Tangshan, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, Juni 2, 2025. (Picha na Liu Mancang/Xinhua)

BEIJING - Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China jana Jumanne zimeonesha kuwa, shughuli za utalii za China zimepata ongezeko kwa hatua madhubuti wakati wa mapumziko ya Sikukuu ya Duanwu ya mwaka 2025, ambapo shughuli za utalii za ndani zikiongezeka kwa asilimia 5.7 kufikia milioni 119 kuliko wakati kama huo wa mwaka uliopita, mapato ya shughuli za utalii yalifikia yuan bilioni 42.73 (Dola za Kimarekani bilioni 5.95), ongezeko la asilimia 5.9 ikilinganishwa na wakati kama huo wa mwaka jana.

Pia ikijulikana kama Sikukuu ya Mashua ya Dragoni, shughuli za utalii za sikukuu hiyo zimehusisha shughuli za jadi za kiutamaduni na shughuli za burudani – zikiwa pamoja na mashindano ya mbio za mashua ya dragoni, ulaji wa zongzi, ambazo ni chakula cha wali wa kunata, maonesho ya uimbaji nyimbo za kienyeji na kusoma mashairi maarufu ya kale.

Makavazi, majengo ya maonesho ya sanaa na shughuli za kiutamaduni nchini kote yamehusisha kutembelea sehemu za mali ya urithi wa utamaduni usioshikika na mila za jadi katika shughuli hizo za utalii za 2025, na hivyo kuongeza furaha ya watembeleaji.

Sikukuu hiyo ya jadi ya Duanwu iliwadia kwa kufuata Siku ya Watoto Juni 1, hivyo watu wa familia nyingi moja moja zimetumia fursa ya mapumziko ya Sikukuu zikisafiri pamoja na watoto wao na kufanya utalii na ziara za masomo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha