99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ujenzi wa handaki la chini ya bahari la Jintang la Reli ya Ningbo-Zhoushan waendelea vema mkoani Zhejiang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2025
Ujenzi wa handaki la chini ya bahari la Jintang la Reli ya Ningbo-Zhoushan waendelea vema mkoani Zhejiang, China
Mafundi kutoka Kampuni ya 14 ya Kundi la Reli la China wakiendesha kreni ndani ya mashine ya ngao ya kuchimba mahandaki ya "Yongzhou" kwenye handaki la chini ya bahari la Jintang la Reli ya Ningbo-Zhoushan katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Mei 29, 2025. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Katika sehemu ya kina chenye urefu wa mita 64 chini ya ardhi, mashine ya ngao ya kuchimba mahandaki ya "Yongzhou" imeanza kazi ya kuchimba handaki la chini ya bahari la Jintang la Reli ya Ningbo-Zhoushan katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China jana Alhamisi.

Handaki hilo la Jintang linaendelea kujengwa kwenye sehemu chini ya bahari yenye urefu wa kilomita 16.18, linaunganisha kisiwa cha Jintang cha Zhoushan na eneo la pwani la Ningbo katika mkoa huo wa Zhejiang na ni muundombinu muhimu kwa njia ya reli ya mwendokasi inayounganisha miji ya Ningbo na Zhoushan katika mkoa huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha