99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mji mdogo wa China watumia mianzi kuhimiza utengenezaji bidhaa rafiki kwa ikolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2025
Mji mdogo wa China watumia mianzi kuhimiza utengenezaji bidhaa rafiki kwa ikolojia
Picha ikionesha msitu wa mianzi mjini Guangde, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (People's Daily Online/Zhang Jun)

Kitu gani huja akilini unapofikiria bidhaa za mianzi? Mkeka, feni… au pengine kitu kingine?

Katika mji wa Guangde, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, unyumbulifu wa matumizi ya mianzi unabadilisha mitazamo ya watu kuhusu utengenezaji bidhaa wa jadi. Vitu vya matumizi ya kila siku kama vile mirija ya kunywea vinywaji, kibodi, kipanya cha kompyuta na nyembe, ambavyo hapo awali vilitengenezwa kwa plastiki, sasa vinatengenezwa kutokana na mianzi. Uwezekano wa matumizi ya nyenzo hii endelevu ni mpana zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali.

Ukiwa unapatikana kwenye makutano ya wilaya nane za Mikoa ya Jiangsu, Zhejiang na Anhui nchini China, Mji wa Guangde unajivunia eneo lenye ukubwa wa karibu mu milioni 1 (hekta 66,667) la misitu ya mianzi, ikisifiwa kuwa "Mji wa Mianzi wa China".

Katika mji mdogo wa Dongting, watu wenyeji hutumia rasilimali kubwa ya mianzi ya mkoa huo. Kuanzia upandaji mpaka uzalishaji na uuzaji, mnyororo unaostawi wa uchakataji umeendelezwa. Mji huo mdogo ni maskani ya kampuni nne kubwa za uchakataji mianzi na zaidi ya karakana 50, ukizalisha bidhaa zenye thamani ya mwaka ya Yuan bilioni 1.3 (dola za Marekani milioni 179) na kutoa zaidi ya nafasi 2,000 za ajira kwa watu wenyeji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha