China yaipongeza Togo kutokana na mafanikio ya kumaliza mpito wa kisiasa
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China inaipongeza Togo kwa kufanikiwa kumaliza mpito wake wa kisiasa.
Bw. Lin ametoa kauli hiyo katika mkutano na wanahabari wakati alipoulizwa maoni yake kuhusu uchaguzi wa rais mpya wa Togo na rais wa kwanza wa Baraza la Mawaziri uliofanyika baada ya marekebisho ya kikatiba yaliyoanza kutekelezwa mwaka 2024 na kuibadilisha rasmi Togo kutoka mfumo wa serikali kuongozwa na rais ambaye baraza lake la mawaziri linawajibika kwa bunge hadi mfumo wa serikali kuundwa na chama chenye viti vingi bungeni.
Bw. Lin amesema, katika mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika 2024, China na Togo ziliboresha uhusiano wa pande mbili hadi uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote, zikifungua ukurasa mpya katika uhusiano wa pande mbili.
Ameongeza kuwa China inatilia maanani uhusiano wake na Togo, ikiwa na nia ya kufanya juhudi pamoja na serikali mpya ya nchi hiyo kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuhimiza maendeleo endelevu ya uhusiano kati ya China na Togo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma