99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

DRC na kundi la M23 waanza duru mpya ya mazungumzo nchini Qatar

(CRI Online) Mei 06, 2025

Duru mpya ya mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 imeanza juzi Jumapili mjini Doha, mji mkuu wa Qatar.

Kwa mujibu wa Redio Okapi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kutokana na mwaliko wa wapatanishaji wa Qatar, wajumbe wa serikali ya DRC na kundi la M23 waliwasili Doha wikiendi iliyopita.

Kundi la M23 limethibitisha kuwasili kwa ujumbe wao mjini Doha, lakini serikali ya DRC bado haijatoa jibu lolote rasmi.

Aprili 23 serikali ya nchi hiyo ilitoa taarifa ikithibitisha kuwa imefikia makubaliano na kundi la M23 juu ya kufanya juhudi za pamoja kuelekea maafikiano yatakayochangia kuanzishwa kwa mchakato wa usimashaji vita kikamilifu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha