99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mwanafunzi wa Tanzania ateuliwa kuwa Balozi wa Huawei wa “Seeds Accelerator” 2025 kwa kanda ya Kusini mwa Afrika

(CRI Online) Mei 06, 2025

Gazeti la “The Citizen” la Tanzania limeripoti habari jana Jumatatu kuwa mwanafunzi wa Tanzania ameteuliwa kuwa Balozi wa Huawei wa “Seeds Accelerator” mwaka 2025 kwa kanda ya Kusini mwa Afrika.

Katika habari hiyo, imeelezwa kuwa mwanafunzi huyo aitwaye Natasha Nassoro anayesomea shahada ya kwanza ya Sayansi katika Uhandisi wa Kielektroniki na Mawasiliano mwaka wa nne, katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), aliteuliwa mwezi uliopita kwenye kambi ya mafunzo ya kimataifa nchini China.

Kambi hiyo iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo ya Huawei mjini Shenzhen inalenga kuhamasisha wanafunzi kwenye masuala ya kidigitali, uvumbuzi, ujasiriamali, na uendelevu.

Akizungumza juu ya kuteuliwa kwake, Nassoro amesema anafurahia kupata uteuzi huo, ambao unamhamasisha kujitahidi zaidi katika masomo na kazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha