

Lugha Nyingine
Uzuri wa Majira: Mwanzo wa Majira ya joto
Habari kila mmoja! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Leo ni Lixia, au Mwanzo wa Majira ya Joto, kipindi cha saba cha vipindi 24 katika Kalenda ya Kilimo ya China na cha kwanza katika majira ya joto. Njoo Kunming, mji wenye kupendeza katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China pamoja nami, na furahia kuanza kwa majira ya joto hapa!
"Vitu vyote hustawi kuanzia siku hii na kuendelea; hivyo basi huitwa 'Mwanzo wa Majira ya Joto.'" Kadri kila siku inaposhuhudia zaidi na zaidi mwanga wa mchana na halijoto kuongezeka, vitu vyote hustawi. Tazama, miti ya Jacaranda kwenye mitaa ya Kunming iko sasa kwenye mchanuo kamilifu!
Wakati wa kipindi hiki, maeneo mengi nchini China bado hushikilia desturi ya kuonja chakula freshi kusherehekea mavuno ya mapema mwa majira ya joto. "Kuonja San Xian" inamaanisha kuonja vyakula mbalimbali vya msimu katika siku hii. Cherry, maharage mapana, na machipukizi freshi ya mianzi kutoka Yunnan ni zawadi kutoka kwa mazingira ya asili wakati wa mpito kutoka majira ya mchipuko hadi majira ya joto.
Uponyaji wa jadi wa Kichina huhusisha majira ya joto na nguvu ya moyo. Kufuatia imani kwamba "vyakula hurutubisha viungo vya mwili vinavyofanana navyo," mayai huchukuliwa kuwa mazuri kwa moyo kwa sababu ya mfanano wao wa umbo. Hii ndiyo sababu baadhi ya sehemu nchini China zina desturi za kula mayai na kucheza michezo ya kupigana mayai wakati majira ya joto yanapoanza.
Jambo la kuvutia, Sikukuu ya Pasaka katika nchi za Magharibi pia inajumuisha shughuli zinazohusiana na mayai, kama kupaka rangi, kuyaficha, kubadilishana na kuwinda Mayai ya Pasaka.
"Mchanuo mdogo wa ua la yungiyungi tayari umeonyesha punde tu ncha yake kidogo, wakati wote kwa mara moja unaona kereng'ende wakitua mauani." Ninaruhusu upepo mwanana kutuma ujumbe wa majira ya joto kwako. Hebu tukumbatie majira hayo kwa shauku na ustawi!
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma