99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China, Russia kufanya maonesho ya sanaa kuadhimisha miaka 80 tangu ushindi wa WWII

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 04, 2025

BEIJING - Maonesho ya sanaa yatafanyika mjini Beijing kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana dhidi ya Ufashisti na kuhimiza mabadilishano ya sanaa kati ya China na Russia.

Maonyesho hayo yenye kaulimbiu ya "Amani na Urafiki -- Kuadhimisha Miaka 80 tangu Ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana dhidi ya Ufashisti," yameandaliwa kwa pamoja na Shirika la Beijing la Urafiki wa Watu kwa Nchi za Nje na Kituo cha Utamaduni wa Russia cha Beijing, miongoni mwa wadau wengine.

Wasanii wenye umri wa miaka 18 hadi 45 kutoka China na Russia wamealikwa kuwasilisha kazi zao. Kipindi cha uwasilishaji kazi za sanaa kitaendelea hadi katikati ya Juni, huku tathmini itafanywa mwishoni mwa Juni. Maonyesho yamepangwa kufanyika katika Jumba la Mnara wa Milenia wa China mjini Beijing kuanzia Agosti 7 hadi 16.

Jumla ya washiriki 80 watapata tuzo, zikiwemo 15 za washindi wa nafasi ya kwanza, 25 za washindi wa nafasi ya pili na washindi 40 wa nafasi ya tatu kutoka kila nchi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha