99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Misri na Sudan zajadili uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda

(CRI Online) April 29, 2025

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan wamefanya mazungumzo mjini Cairo kuhusu maendeleo mapya ya hali ya Sudan na njia za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Misri, mkutano huo uliangazia mabadiliko mapya yaliyoshuhudiwa katika hali ya Sudan na maendeleo ambayo Jeshi la Sudan (SAF) limepata katika kurejesha udhibiti wa mji mkuu Khartoum.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu haja ya kuongeza juhudi za kutoa uungaji mkono na msaada hitajika kwa watu wa Sudan kwenye maeneo yaliyoathirika kwa vita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha