99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

AU yapeleka Jopo la Washauri kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini Sudan Kusini

(CRI Online) April 02, 2025

Umoja wa Afrika unapanga kupeleka ujumbe wa ngazi ya juu wa Jopo la Washauri mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, kushughulikia mgogoro unaoendelea nchini humo na kusababisha ukosefu wa usalama.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema, Jopo hilo litafanya majadiliano na wadau wote ili kuboresha juhudi za upatanishi na kuunga mkono utekelezaji kamili wa Makubaliano Yaliyohuishwa ya Mgogoro wa Sudan Kusini (A-ARCSS).

Taarifa hiyo imesema, Umoja wa Afrika unahimiza pande zote husika kudumisha mapendekezo ya Makubaliano hayo, na kwamba Umoja huo unaendelea kushirikiana na washirika wa kikanda na kimataifa, ikiwemo Mamlaka ya Kiserikali juu ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Mataifa ili kuunga mkono mpito wa Sudan Kusini kuelekea amani ya kudumu na demokrasia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha