

Lugha Nyingine
China yaainisha kazi muhimu kuzidisha mageuzi ya vijiji na kuhimiza ustawishaji wa vijiji
BEIJING - China imetangaza "waraka wa nambari " wa serikali kuu wa mwaka 2025 siku ya Jumapili, ukielezea majukumu muhimu ya kuendeleza kwa kina mageuzi ya vijiji na hatua madhubuti za kuendeleza ustawishaji wa vijiji kwa pande zote.
Waraka huo ukiwa taarifa ya kwanza ya sera inayotolewa na China kila mwaka, unachukuliwa kuwa viainishi vya sera muhimu, vikihusisha majukumu muhimu ya sehemu sita kubwa: kuhakikisha utoaji wa nafaka na mazao mengine muhimu ya kilimo, kuimarisha mafanikio ya kuondokana na umaskini, kuendeleza viwanda vya maeneo ya vijiji, kuhimiza ujenzi wa vijiji , kukamilisha mfumo wa utawala vijijini, na kuboresha mfumo wa ugawaji rasilimali vijijini.
Waraka huo unatoa wito wa kuongeza nguvu ya kazi zinazohusiana na kilimo mwaka 2025 na baadaye, na kuweka malengo ya kustawisha vijiji kwa pande zote na kuimarisha msingi wa kazi ya kilimo.
Waraka huo unasema, "Kuchukulia mageuzi, ufunguaji mlango, na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia kuwa msukumo, ili kulinda usalama wa nafaka na kuhakikisha hali ya watu wengi kukumbwa na umaskini haitatokea, au walioondokana na umaskini hawatarudi tena katika hali ya umaskini."
Waraka huo unasisitiza kuwa, nchi ya China itafanya kila jitihada kuongeza ufanisi wa kilimo, kuleta hamasa kubwa katika maeneo ya vijijini na kuongeza mapato ya kilimo, hivyo kuweka msingi imara wa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Waraka unasisitiza umuhimu wa kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora katika kilimo kwa kuzingatia hali ya eneo husika. Pia unatoa wito wa kuanzisha viwanda vya ongozi vya teknolojia ya hali ya juu za kilimo, na kuongeza kasi ya mafanikio katika aina mbalimbali za mazao.
Waraka huo unasema “China itaunga mkono maendeleo ya kilimo bora cha kisasa na kupanua wigo wa matumizi ya teknolojia ya AI , data kubwa na mfumo wa uchumi wa anga ya chini".
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma