

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika watoa wito wa kusimamishwa mara moja kwa mapigano mashariki mwa DRC
Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito wa kusimamishwa mara moja bila ya masharti kwa mapigano na kundi la waasi wa M23 na makundi mengine yenye silaha kuondoka haraka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kauli hiyo imetolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo katika taarifa iliyotolewa Jumanne wiki ya wiki hii kufuatia mkutano wake wa hivi karibuni kuhusu kuongezeka kwa mapigano katika eneo hilo la mashariki mwa DRC.
Baraza hilo huku likieleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu inayoendelea kuwa mbaya mashariki mwa DRC, limesema hali hiyo inahitaji hatua za pamoja katika moyo wa "Masuluhisho ya Afrika kwa matatizo ya Afrika.”
Pia Baraza hilo limeeleza umuhimu wa kutafuta chanzo halisi cha mgogoro huo, ikiwemo matumizi yasiyo halali ya rasilimali za asili, na kuahidi kuendelea na juhudi za kutatua mgogoro huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma