99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Afrika Kusini yateua waendeshaji biashara za utalii ?65 kushughulikia viza kwa watalii wa China na India

(CRI Online) Januari 14, 2025

Serikali ya Afrika Kusini imeteua waendeshaji biashara za utalii 65 watakaoshughulika na utoaji viza kwa watalii kutoka China na India.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini imetangaza kukamilika kwa mchakato huo wa kuteua kundi la kwanza la kampuni 65 za huduma za utalii kati ya kampuni zote 141 zilizowasilisha ombi la kujiunga na Mpango wa Waendeshaji Biashara za Utalii Wanaoaminika (TTOS), unaolenga kuvutia zaidi watalii kutoka China na India.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini Leon Schreiber amesema anatarajia kukaribisha ujio wa wimbi la kwanza la watalii chini ya mpango huo wa TTOS ndani ya wiki kadhaa, ikiwa ni hatua madhubuti ya kuonesha jinsi serikali ya awamu ya saba inavyofanya kazi pamoja kuleta mageuzi halisi na ukuaji wa uchumi ili kuongeza ajira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha