99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Abiria wanusurika kwenye ajali ya treni kugongana na lori Kusini mwa Zambia

(CRI Online) Desemba 25, 2024

Abiria wa treni moja wamenusurika bila kujeruhiwa baada ya treni yao kugongana na lori kwenye eneo la Choma kusini mwa Zambia jana Jumanne.

Ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara na reli, baada ya treni iliyokuwa ikielekea Kaskazini kugongana na lori na trela lililobeba vigae vya sakafu likielekea Afrika Kusini.

Ofisa mahusiano wa Shirika la Reli Zambia, Sombe Longwani-Ngo’nga, amesema uchunguzi wa awali umedokeza kuwa dereva wa lori alishindwa kusimama mbele ya makutano na kusababisha ajali hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha