99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu watano katika mji wa pwani wa Kenya

(CRI Online) Desemba 03, 2024

Afisa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto katika Kaunti ya Mombasa nchini Kenya Bw. Ebrahim Basafar amesema watu watano wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa kizingiti kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

Bw. Basafar amesema walipigiwa simu na kwenda kushughulikia ukuta huo ulioangushwa na mvua, na kugundua kwamba watu watatu walikuwa wamefariki papo hapo, na wengine wawili walifariki wakipatiwa matibabu hospitalini akiwemo mtoto mmoja.

Ajali hiyo imetokea siku mbili zilizopita baada ya serikali kutoa tahadhari ya mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha katika maeneo kadhaa nchini Kenya.

Mvua hizo zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu, na kingo za mito mingi zimevunjika na mamia ya watu wamepoteza makazi yao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha