99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Marekani yapiga tena kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama ?juu ya mswada wa azimio wa kusimamisha vita Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2024

Naibu Mwakilishi wa Mambo Maalumu ya Kisiasa wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Robert Wood (katikati, mbele) akipiga kura ya turufu  juu ya mswada wa azimio la Baraza la Usalama  la kusimamisha vita mara moja huko Gaza kwenye makao mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York, Novemba 20, 2024. (Xinhua/Xie E)

Naibu Mwakilishi wa Mambo Maalumu ya Kisiasa wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Robert Wood (katikati, mbele) akipiga kura ya turufu juu ya mswada wa azimio la Baraza la Usalama la kusimamisha vita mara moja huko Gaza kwenye makao mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York, Novemba 20, 2024. (Xinhua/Xie E)

Tarehe 20, Marekani imepiga tena kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mswada wa azimio la kutaka kusimamisha vita mara moja huko Gaza

Siku hiyo Baraza la Usalama lilipiga kura juu ya mswada wa azimio uliotolewa na nchi 10 zisizo wajumbe wa kudumu wa baraza hilo. Mswada huo wa azimio unataka usimamishaji vita wa mara moja ulio wa kudumu bila ya masharti yoyote katika kanda ya Gaza, na kuwaachilia huru watu wote wanaotiwa mbaroni. Nchi wajumbe 14 kati ya 15 wa baraza hilo zimepiga kura za ndiyo, huku Marekani ikiwa nchi mjumbe wa kudumu ikipiga kura ya turufu, ambayo imesababisha mswada huo wa azimio kushindwa kupitishwa.

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Fu Cong alisema kwenye hotuba yake ya ufafanuzi baada ya upigaji kura, kwamba upande wa China umesikitishwa sana kwa matokeo hayo, na unatoa wito wa kuitaka Marekani uzingatie kwa makini wajibu wake wa nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, kuunga mkono baraza hilo kuchukua hatua zote za lazima kwa ajili ya kusimamisha vita mara moja , kuokoa maisha na kurejesha hali ya amani.

Tangu raundi mpya ya mgogoro kati ya Palestina na Israeli ilipolipuka Oktoba mwaka jana, operesheni za kijeshi za Israeli zimesababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 40,000 katika kanda ya Gaza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha