99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Huawei kushirikiana na kampuni ya Kenya kwenye ufumbuzi wa huduma kwa teknolojia ya akili bandia

(CRI Online) Novemba 20, 2024

Kampuni ya teknolojia ya China Huawei imesaini makubaliano na kampuni ya bima ya Kupa Kenya ili kutoa ufumbuzi wa huduma kwa wateja kwa teknolojia ya akili bandia (AICC).

Ofisa mkuu mtendaji wa Kupa Kenya, John Onyango Otolo, aliviambia vyombo vya habari kuwa ufumbuzi wa teknolojia kutoka Huawei utawezesha kampuni yake kuongeza kwa kiasi kikubwa uzoefu kwa wateja. Pia ushirikiano wao utaboresha ufanisi wa gharama kwa kuwawezesha kuhudumia wateja wengi kwa kutumia wafanyakazi wachache. Aidha amesema teknolojia hiyo itatekelezwa kwa awamu na kurekebishwa ili kusaidia lugha za ndani na kuhudumia wateja wengi zaidi.

Naye mkurugenzi wa uwasilishaji na huduma wa Huawei Kenya, Lin Xiaonan, alisema kuwa ufumbuzi wa AICC unaoandaliwa na Huawei utawezesha Kupa Kenya kupanua shughuli zake za kituo cha simu na hivyo kuhudumia wateja wengi zaidi kwa ufanisi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha