99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mgogoro wa Sudan waacha?watoto zaidi milioni 15?nje ya mfumo wa shule

(CRI Online) Novemba 13, 2024

Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Ustawi wa Watoto la Sudan Bw. Abdul Qadir Abdullah Abu amesema watoto zaidi milioni 15 nchini Sudan wako nje ya mfumo wa shule.

Akiongea mjini Port Sudan Bw. Abu amevishutumu Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) kwa ukiukaji wa kimfumo dhidi ya haki za watoto, akidai kuwa wanamgambo hao wameteka nyara watoto zaidi 2,500.

Ameongeza kuwa watoto karibu 3,000 wameuawa wakiwa ukimbizini, na watoto zaidi ya 8,000 wamekuwa wakitumikishwa na vikosi hivyo kwenye mapigano.

Bw. Abu amesema watoto ndiyo "kundi lililo hatarini zaidi" na wanahitaji mifumo ya ulinzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha